Je, tukusaidie?

You can always Contact Us – but before you do, take a moment to scan our list of Frequently Asked Questions. The answer you’re looking for could be right here…

Nahitaji kubeba nini nikienda kuchukua gari?

Dereva mkuu anahitaji mambo matatu (yote yakiwa kwa jina lao wenyewe):

 1. Kadi ya malipo yenye mjazo wa kutosha ya kusimamia amana ya gari
 2. Leseni Kamili ya Uendeshaji gari, ambayo wamekuwa nayo kwa miaka miwili iliyopita
 3. Rentalcars.com Vocha ya Ukodeshaji, au eVocha kwenye app yetu

Madereva wa ziada watahitaji leseni kamili ya uendeshaji gari.

Utalipia madereva wowote wa ziada na chombo cha ziada utakapofika kuchukua gari – kwa hivyo ni muhimu kutilia maanani hizo gharama unapofikiria kuhusu kadi yako ya malipo. Kiasi cha amana utakipata kwenye sheria na masharti ya gari na kwenye vocha yako ya ukodeshaji.

Naweza kukodesha gari ikiwa sina credit card?

La, kwa bahati mbaya – karibu katika visa vyote utahitaji kadi ya malipo.

Kampuni ya ukodeshaji gari itaweka amana kwenye kadi ya malipo ya dereva mkuukabla yao kupeana funguo za lile gari la kukodesha. Bila kadi ya malipo, hawawezi kuchukua ile amana, kwa hivyo hawatakupa funguo.

Utaweza kujua ikiwa unahitaji kadi ya malipo kwenye sheria na masharti ya gari lako, katika ‘Unachohitaji katika uchukuaji gari’.

Naweza kurekebisha utumaji ombi wangu jinsi gani/ kuongezea nambari yangu ya safari ya ndege?

Chagua ‘Thibiti utumaji maombi’ kwenye ukurasa wetu wa nyumbani. Unaweza kubadilisha umbali wa safari yako, aina ya gari unayotaka na uongezee maelezo kama vile nambari ya safari yako ya ndege.

Hatulipishi ada yoyote ya usimamizi ya kubadilisha kwako kwa utumaji ombi. Lakini ikiwa utabadilisha utumaji ombi wako kwa namna yoyote, kuna uwezekano kwamba bei itabadilika.

Ni wazo nzuri kufanya mabadiliko yoyote mapema iwezekanavyo. Tutaweka bidii zaidi, lakini wakati mwingine yale makampuni ya ukodeshaji gari tunayofanya kazi nayo huwa hayapokei vyema mabadiliko yanayofanywa kwa ilani ya mda mfupi kabla ya safari kuanza.

Ni njia gani za malipo ambazo Rentalcars.com hukubali?

Unaweza kutuma maombi ya gari lako kwetu kwa kutumia nyingi za kadi za malipo. Tutakufahamisha nini tunakubali wakati wa kutuma ombi.

Lakini ni muhimu kukufahamisha kwamba yule dereva mkuu atahitaji awe na kadi ya malipo ili aweze kuchukua gari. Hii ni kwa sababu kampuni ya ukodeshaji gari itahitaji kuweka amana kwenye kadi ya malipo ya dereva mkuu.

Unaweza kulipia ukodeshaji wako kwenye tovuti yetu vyovyote utakavyokufaa – sio lazima utumie kadi ile ile ili kutuma ombi la ukodeshaji wako wa gari na kulipa amana.

Nawezaje kubatilisha utumaji ombi wangu?

Ili kubatilisha utumaji maombi wako, nenda kwa 'Thibiti utumaji maombi', ingiza maelezo yako na ubatilishe utumaji ombi wako.

Ikiwa unahitaji kubadilisha mipango yako na ungali ungependa kukodisha gari, unaweza kwenda kwa 'Thibiti Utumaji maombi' na badala yake urekebishe utumaji ombi wako.

Sera ya ubatilishaji ni gani?

Ikiwa utabatilisha ZAIDI ya saa 48 kabla ya ukodeshaji wako kufika, utapokea rejesho la pesa zako Walakini, ikiwa ulilipa amana wakati ulituma ombi la ga gari, hautapata kurejeshewa ile amana.

Ikiwa utabatilisha CHINI ya saa 48 kabla ya ukodeshaji wako kuanza, utapata kurejeshewa pesa zako, lakini zikiwa zimeondolewa bei ya ukodeshaji wa siku tatu.

Ikiwa ulikuwa umelipa amana ulipotuma ombi la gari, utapokea rejesheo la pesa zikiwa zimeondolewa ama amana au gharama ya ukodeshaji wa siku tatu – yoyote iliyo ya gharama kubwa zaidi.

Ikiwa ukodeshaji wako ulikuwa wa chini ya siku tatu, hatutapokea rejesheo lolote. Hii pia itakuwa vivyo hivyo ikiwa utatupigia simu ili kubatilisha utumaji ombi wako kwenye ile kaunta ya ukodeshaji gari.

Ikiwa utabatilisha BAADA ya ukodeshaji wako kuanza, hautapokea rejesho la pesa.

Ikiwa hautachukua gari (inavyojulikana kwa kawaida kama ‘kutojitokeza’), hautapata rejesho la pesa.

Makampuni ya ukodeshaji gari huiita ‘kutojitokeza’ ambapo unakosa kuchukua gari kwa sababu (kwa mfano): Hauwasili ile siku na saa iliyopangwa, hauna stakabadhi zinazofaa, au haustahiki kukodeshewa, au yule dereva mkuu hana kadi yake ya malipo yenye mjazo wa kutosha ya kuweka amana.

Baadhi ya makampuni ya ukodeshaji magari yana sera yao ya ubatilishaji, ambayo utaipata kwenye sheria na masharti ya utumaji maombi wako.

Yanilazimu kulipia madereva wa ziada?

Utalilipa lile kampuni la ukodeshaji gari kwa ajili ya dereva yeyote wa ziada unayemhitaji, wakati unapochukua gari.

Unaweza kuchagua kuongezea dereva wa ziada mwanzoni wakati unapotuma ombi la gari lako, au uende kwa 'Thibiti Utumaji Maombi' na Urekebishe utumaji wako wa maombi ili kuongezea dereva mwingine.

Itanilazimu kulipia ada za ziada kwenye kaunta ya ukodeshaji?

Ndio, nyakati zingine utaweza.

Utalipa amana ya gari lako na chochote xha ziada au madereva wa ziada unaotaka.

Ada zingine zitategemea na mahali unakokodeshea, umri wa (ma)dereva, na yale safari yako unahusisha. Hii hapa baadhi ya mifano ya mabadiliko ambayo huenda yakatokea:

Sheria na kodi ya Serikali, Ada za eneo, ada ya safari ya kuelekea upande mmoja, ada ya mafuta, ada ya kadi ya malipo, ada za kustahimili masika, dereva mchanga, dereva mkongwe, saa zisizo za wakati wa kazi, usaidizi wa kando ya barabara, maili na ada ya kuvuka mpaka wa nchi.

Kwa maelezo zaidi unaweza kuangalia sheria na masharti ya gari lako.

Hitajio za leseni ya uendeshaji gari ni gani?

Utahitaji kubeba leseni yako ya uendeshaji gari ili kwenda kuchukua gari lako la ukodeshaji.

Makampuni ya ukodeshaji gari hutaraji madereva wawe wamekuwa na leseni yao ya uendeshaji gari kwa mda usiopungua miaka miwili. Leseni za mda hazikubaliwi.

Wakati unapokodesha gari ng'ambo katika baadhi ya mataifa utahitaji Kibali cha Kimataifa cha Uendeshaji gari, pamoja na leseni yako ya uendeshaji gari. Vocha ya Ukodeshaji tutakayo kutumia baada ya kutuma ombi itakufahamisha ikiwa unahitaji hicho Kibali cha Kimataifa cha Uendeshaji gari kwa ajili ya safari yako.

Ikiwa una leseni ya uendeshaji gari ya Uingereza na unakodesha gari ndani ya Uingereza, huenda ukaitishwa msibo kwenye ile kaunta ya ukodeshaji gari. Unaweza kufahamu mengi zaidi hapa.

Nitalipiaje chombo cha ziada?

Utalilipa lile kampuni la ukodeshaji gari kwa chochote cha ziada unachohitaji – kama vile kiti cha mtoto cha gari, GPS au minyororo ya gari kwenye theluji – wakati utakapokuwa ukichukua gari.

Ikiwa ungetaka kuongezea chombo cha ziada baada ya kutuma ombi lako, unaweza kwenda kwa 'Thibiti Utumaji Maombi' na uchague 'Rekebisha' ili kuongezea unachohitaji.

Kwa sababu lile kampuni la ukodeshaji gari litachukua malipo moja kwa moja ya chochote cha ziada utakachochagua, kwa bahati mbaya hatuwezi kukuhakikishia kuwa watakuwa na chochote kile utakachoitisha.

Kuna baadhi ya magari ambayo unaweza kulipia vitu vya ziada, na kwa hivyo tuneaweza kukuhakikishia kwamba utayapata. Tutakounyesha ikiwa hilo linapatikana kwenye gari lako la ukodeshaji. Tunashughulikia uwezekano huo – tunajua linaweza kufanya mambo kuwa rahisi zaidi, kwa hivyo tunatarajia kulipanua.

Nitaitishaje ankara au risiti?

Unaweza kupata risiti au nakara wakati wowote kwa kwenda kwa 'Thibiti Utumaji Maombi' na kuchagua risiti.

Ikiwa ungependa mabadiliko yoyote yafanywe kwenye ankara au risiti yako, tafadhali wasiliana nasi.

Na je, nikitaka kupeleka gari lililokodeshwa katika nchi nyingine?

Ikiwa ungependa kuchuka gari lako kwenye nchi moja na kisha ulirejeshe kwenye nchi nyingine, matokeo ya utafutaji wako yatakuonyesha yale magari unayoweza kufanya hivyo kwayo.

Ikiwa unapanga kuvuka mpaka wowote wa nchi wakati wa safari yako, tilia maanani:

 1. Huenda ikakubidi kulipa zaidi

  Mara nyingi huwa kuna ada za ziada, kodi au usimamiaji wa ziada utakaolipa kwenye kaunta ya ukodeshaji gari.

 2. Huenda isiwezekane

  kulingana na ni wapi unakokodeshea, huenda usiweze kulipeleka gari lako hadi nchi nyingine.

Tafadhali wasiliana nasi ikiwa ungependa kupeleka gari lako hadi nchi nyingine wakati wa safari yako, nasi tutakuelezea chugua zilizopo moja kwa moja.

Na je, ikiwa nina maswali baada ya ukodeshaji wangu kuisha?

Tafadhali chagua sehemu ya Baada ya ukodeshaji iliyoko hapa chini, ingiza maelezo ya utumaji maombi wako, jaza kwenye fomu nasi tutaiangalia.

Sera ya mafuta ni nini?

Sheria ya mafuta kwa ajili ya ukodeshaji wako inaeleza jinsi utakavyolipa mafuta ya ukodeshaji wako wa gari, na ikiwa utahitaji kujaza tanki kabla ya kurejesha gari.

Unaweza kupata sheria ya mafuta ya kila gari wazi wazi kwa maelezo yake. Mengi ya magri huja na sheria ya mafuta ya 'Jaza lijae', ambalo ndilo chaguo lisilo na gharama kubwa. Tanki litakuwa limejazwa utakapokuwa ukichukua gari, na utalirejesha likiwa limejazwa.

Ni usimamiaji upi wa ziada ambao Rentalcars.com itanipatia?

Tunapeana Bima Kamili kwa Rentalcars.com, ambayo itakurejeshea pesa pesa zako ikiwa gari lako la ukodeshaji litaharibika au kuibiwa na kampuni yako ya ukodeshaji gari liweke amana yako au likulipishe ada ya ziada kwa ajili ya uharibifu.

Bima Kamili husimamia amana unayowacha unapochukua gari, yale ya ziada, sehemu zote za nje ya gari ambazo hazisimamiwi na ule usimamiaji wa kimsingi ambao gari lako la ukodeshaji huwa nao, na pia ada zozote za ukokotwaji au usimamizi ambazo huenda ukatozwa. Fahamu mengi zaidi kuhusu Rentalcars.com Full Protection

Na je, ikiwa sikupokea uthibitisho wa utumaji ombi wangu?

Huwa tunakubalia mengi ya maombi yaliyotumwa moja kwa moja, na karibu yote ndani ya saa 48. Ikiwa hatujakubali utumaji ombi wako ndani ya saa 48, kisha tutawasiliana nawe kukuelezea ni kwanini.

Unaweza kuangalia hali ya utumaji ombi wako baada ya kukubaliwa katika 'Thibiti Utumaji Maombi'.

Ikiwa uliweka amana mwanzoni ulipotuma mombi, utapokea Vocha yako ya Ukodeshaji mara utakapolipia kikamilifu utumaji maombi wako wa ukodeshaji gari.

Ni wapi nitapata kujua kuhusu bima au usimamiaji wa gari langu la kukodesha?

Utapata usimamiaji unaokuja na gari lako la ukodeshaji na orodhesho la sheria na masharti. Utayaona haya kwenye matokeo ya utafutaji wako katika 'Sheria na Masharti', na kwenye gari katika 'taarifa muhimu' utapata 'Sheria na Masharti Kamili' pale chini.

Usimamiaji wowote ambao huja kama wa kawaida hupeanwa na hili kampuni la ukodeshaji gari. Utayapata maelezo ya usimamiaji huu kwenye makubaliano ya ukodeshaji utakayotia sahihi utakapochukua gari.

Gari langu la kukodesha lina bima gani?

Ukodeshaji wote lazima uwe na Ondoleo la Gharama ya Uharibifu kwa Mgongano na Bima dhidi ya Wizi. Kwa kulingana na mahali unapokodeshea vitu hivi:

 • Vitajumuishwa kwenye gari utakapotuma ombi lake au
 • Kupeanwa na kampuni ya kadi ya malipo ya dereva mkuu, au
 • Kununuliwa kutoka kwa hii kampuni ya ukodeshaji gari utakapoenda kuchukua gari

Unaweza kupata maelezo ya yote yanayojumuishwa kwenye ukodeshaji wako kwenye sheria na masharti na pia kwenye vocha yako ya ukodeshaji.

Naweza kurejeshewa pesa ikiwa nitarejesha gari langu mapema?

Kwa bahati mbaya, hatuwezi kukurejeshea pesa zako kwa sehemu yoyote ya ukodeshaji wako ambao haukuutumia.

Hii ni kwa sababu tutakuwa tumejipeana kikamilifu kwa niaba yako, na kampuni ya ukodeshaji gari itakuwa ikitarajia lile gari litumike kwa mda wote. Watakuwa wametayarisha magari yao na mahitaji ya maegesho kuhusiana na utumaji ombi wa asili.

Excess ni nini?

La ziada ni kiasi cha pesa utakachohitaji kulipa ikiwa gari litaharibika (wakati limesimamiwa katika Ondoleo la Gharama ya Uharibifu kwa Mgongano) au kuibiwa (wakati limesimamiwa katika Bima dhidi ya Wizi).

Unaweza kupata maelezo ya ada za ziada kwa ajili ya ukodeshaji wako kwenye sheria na masharti na kwenye vocha yako ya ukodeshaji.

Ondoleo la Gharama kutokana na Mgongano au CDW ni nini?

Ondoleo la Gharama ya Uharibifu kwa Mgonganorni aina ya usimamiaji kwa magari ya ukodeshaji. Huwekea mipaka ugharamikiaji wa dereva ikiwa lile gari la kukodesha litaharibika.

Hii inamaanisha kwamba kampuni ya ukodeshaji gari haitakulipisha gharama yote nzima ikiwa gari litaharibika ukiwa nalo.

Mara nyingi huwa kuna ada za ziada, ambapo inamaanisha kwamba utalipa sehemu ya kwanza ya gharama ya urekebishaji.

Maelezo ya kina kuhusu kile Ondoleo la Gharama ya Uharibifu kwa Mgongano hujumuisha hutegemea kampuni ya ukodeshaj gari unakokodesha gari.

Lakini kwa kawaida huwa haihusishi vioo vya mbele vya gari, magurudumu, chini ya gari, kufuli za kubadilisha, funguo za kubadilisha na ada za kukokotwa. Hii inamaanisha kwamba ikiwa hizi sehemu za gari zitaharibika, au gari lako limekokotwa, utagharamikia gharama yote, na wala sio ada ya ziada tu.

Pia Ondoleo la Gharama ya Uharibifu kwa Mgongano hufanyakazi tu ikiwa utadumisha sheria na masharti ya makubaliano ya ukodeshaji (ambayo utatia sahihi wakati unapochukua gari). Hii inamaanisha kwamba ikiwa (kwa mfano) utaendesha gari ukiwa mlevi au kuegesha mahali hatari kisha gari liharibiwe, utagharamikia gharama yote ya urekebishaji, na wala sio ada ya ziada tu.

TP au Bima dhidi ya Wizi ni nini?

Bima dhidi ya Wizini aina ya usimamiaji kwa magari ya ukodeshaji. Huwekea mipaka ugharamikiaji wa dereva ikiwa lile gari la kukodesha litaibiwa.

Hii inamaanisha kwamba kampuni ya ukodeshaji gari haitakulipisha gharama yote nzima ikiwa gari litaibiwa ukiwa nalo.

Mara nyingi huwa kuna ada za ziada, ambapo inamaanisha kwamba utalipa sehemu ya kwanza ya gharama ya urekebishaji au ununuzi wa vipuri.

Maelezo ya kina kuhusu kile Bima dhidi ya Wizi hujumuisha hutegemea kampuni ya ukodeshaj gari unakokodesha gari.

Bima dhidi ya Wizi hufanyakazi tu ikiwa utadumisha sheria na masharti ya makubaliano ya ukodeshaji (ambayo utatia sahihi wakati unapochukua gari). Hii inamaanisha kwamba ikiwa (kwa mfano) utaliacha gari huku halijafungwa na liibiwe, utagharamikia gharama yote ya urekebishaji au ununuaji wa vipuri, na wala sio ada ya ziada tu.

Ninafaa kufanya nini nitakapofika kwenye gari langu?
 1. Kagua gari

  Zinguka gari kotekote na uangalie ndani, ukitafuta uharibifu. Ikiwa utapata uharibifu wowote, muulize ajenti wa kuampuni ya ukodeshaji gari anakili kwenye makubaliano yako ya ukodeshaji. Piga picha ili uwe na uhakika wa jinsi gari lilivyokuwa pale mwanzo.

 2. Kagua aina ya mafuta linayotumia

  Fungua funiko na uangalie ikiwa huwa latumia petroli au dizeli. Huenda Petroli ikawa na ‘95’ juu yake. Ikiwa huna uhakika na aina ya mafuta gari lako hutumia, muulize ajenti kabla haujaondoka.

 3. Angali kwenye dashibodi

  Mafuta ya gari la ukodeshaji huwa yanapeanwa kwa misingi ya ‘Jaza lijae’, ambapo inamaanisha kwamba unaanza kwa tanki lililojaa kikamilifu na unarejeshe gari likiwa limejazwa tanki kikamilifu. Gurumisha kwa funguo ili kuangalia kama tanki limejaa kikamilifu (na taa za mbele zinafanya kazi).

 4. Kagua njia ikiwa

  Ikiwa gari lako lina GPS, ni bora zaidi kuiweka katika lugha yako kabla haujaondoka.

 5. Chukua mda

  Mara kila mmoja amefunga mshipi wa usalama, chukua dakika ili take a minute to adjust the mirrors, move the seat, find reverse and check where the indicators are.

 6. Look out for a petrol station

  When you’re heading off, look out for a petrol station. Itazuia usumbufu wa dakika za mwisho mwisho za kujaza gari mafuta kabla haujalirejesha.

Mbona inanibidi nitie sahihi makubaliano ya ukodeshaji kwenye kaunta?

Kwa kuwa kandarasi unayotia sahihi inaelezea yale unayokubaliana nayo unapokodisha gari kutoka kwa ile kampuni ya ukodeshaji gari.

Rentalcars.com hujiendesha kama wakala au ajenti tu. Sisi huunganisha wateja na makampuni ya ukodeshaji gari, na kupokea maombi. Yale makubaliano ya ukodeshaji unayotia sahihi ni tofauti kulingana na kampuni ya ukodeshaji gari na nchi unakokodesha gari.

Kama ilivyo na kandarasi nyingine yoyote unayotia sahihi, daima ni muhimu kuhakikisha unafahamu wa na unaridhika na yale unayokubaliana nayo.

Ninawezaje kuzuia ada za ziada nitakaporejesha gari?

Kwa kurejesha gari kwa wakati unaofaa, likiwa na kiasi sawa cha mafuta na bila uharibifu wowote au chafu kupindukia.

Wakati unaporejesha gari, huenda kampuni ya ukodeshaji gari ikakulipisha kwa ajili ya:

 • siku nzima ya ziada ikiwa utarejesha gari kama umechelewa
 • kujaza upya mafuta, na ada ya kutekeleza hilo
 • kubidi kulisafisha gari iwapo liko chafu kupindukia
 • uharibifu mpya
Nitafanya nini ikiwa gari langu litaharibika, au ikiwa nitahusika katika ajali?

Ikiwa gari litaharibika, pigia simu kampuni ya ukodeshaji gari kwa nambari zao za dharura maramoja. Utaipata hiyo nambari kwenye makubaliano ya ukodeshaji uliyotia sahihi ulipochukua gari.

Kampuni ya ukodeshaji gari itakueleza utakachofanya baada ya hapo.

Hifadhi salama nyaraka zozote unazopewa.

Ikiwa utapatwa na ajali, piga simu kwa nambari ya dharura ya kampuni ya ukodeshaji. Utaipata hiyo nambari kwenye makubaliano ya ukodeshaji uliyotia sahihi ulipochukua gari.

Pigia polisi simu ili kuripoti hiyo ajali.

Kampuni ya ukodeshaji gari itakuuliza ujaze fomu ya ripoti ya ajali baadaye.

Nimetozwa ada gani na kampuni yangu ya ukodeshaji gari?

Kuna sababu chache za ni kwanini kampuni ya ukodeshaji gari huenda ikakulipisha moja kwa moja.

Wakati unapochukua gari, utailipa kampuni ya ukodeshaji gari kwa ajili ya madereva wowote wa ziada na chombo cha ziada.

Ikiwa utamua kununua Bima Kamili ya Rentalcars.com, tutakupa ule usimamiaji na utatulipa wakati unapotuma ombi. Ukiamua kununua usimamiaji pale kwenye kaunta wakati unapochukua gari, lile kampuni la ukodeshaji gari litapeana usimamiaji na utawalipa moja kwa moja. Usimamiaji wa gari la kukodesha ni jambo tata na tunajua linaweza kuwa la kutatanisha. Fahamu mengi zaidi kuhusu Rentalcars.com Bima kamili.

Baada ya ukodeshaji wako, kampuni ya ukodehsji huenda ikakulipisha kujaza upya mafuta, tiketi za uegeshaji, faini au uharibifu kwenye gari.

Wanafaa kuorodhesha ada zozote kwenye zile nyaraka wanazokupea (isipokuwa baadhi ya faini na tiketi za uegesho huena zikafika baadaye).

Ikiwa haufahamu zile nyaraka ambazo umepewa, au hauna uhakika ni kwanini umelipishwa, tafadhali wasiliana kwenye sehemu ya [Baada ya ukodeshaji] iliyo hapa chini na tutaweza kuangalia.

Nitaunda Akaunti namna gani?

Nenda kwa Ili Kuingia kwenye tovuti yetu na uchague Jenga akaunti.

Unachohitaji ili kujenga akaunti ni anwani ya baruapepe na nenosiri. Kisah tutakutumia baruapepe ya kuthibitisha akaunti yako.

Mara baada ya akaunti yako kuanzishwa, unaweza kuingia na kufuatilia utumaji maombi wako wote.

Na je, ikiwa ningetaka kuchukua au kurejesha gari langu la kukodesha nje ya masaa ya kazi?

Tutakuuliza ni lini ungetaka kuchukua gari na kurejesha gari lako la kukodeshwa utakapokuwa ukitafuta gari. Kisha tutakuonyeha yale magari mabayo yanapatikana katika zile nyakati unapohitaji. Ikiwa hakuna magari yoyote, tutapendekeza chaguo zinazokaribiana kwa karibu na yale unayohitaji.

Ikiwa mipango yako itabadilika baada ya wewe kutuma ombi, unaweza kubadilisha saa zako za kuchukua na kurejesha gari kwenye Thibiti utumaji maombi na tutakuonyesha yale yanayopatikana katika hizo saa zako mpya.

Baadhi ya makampuni ya ukodeshaji magari hupeana huduma nje ya saa za kazi katika maeneo kadha, lakini yatalipisha ada za ziada kwa hilo. Makampuni mengine ya ukodeshaji gari hayawezi kupeana huduma ya nje ya saa za kazi .

Ikiwa kuna suala lolote kuhusiana na huduma ya nje ya saa za kazi katika utumaji maombi wako, tutawasiliana nawe.

Nini kitafanyika ikiwa safari yangu ya ndege itahairishwa au kubatilishwa?

Ikiwa uliongezea maelezo yako ya safari ya ndege kwenye utumaji maombi wako, kampuni ya ukodeshaji gari litaweza kufuatilia safari yako ya ndege na huenda ikakudhikilia lile gari hadi kufikia mda wa saa moja.

Ikiwa safari yako ya ndege itacheleweshwa na haukuongezea maelezo yako ya safari ya ndege kwenye utumaji maombi wako, tafadhali tupigie simu ukitumia ile nambari ya simu iliyo kwenye Vocha yako ya Ukodeshaji haraka iwezekanavyo.

Ucheleweshwaji wa safari ya ndege na ubatilishaji ni mambo tusiyoweza kuthibiti, kwa hivyo kwa bahati mbaya Rentalcars.com haiwezi kuwajibikia shid zozote au gharama zenye kusababishwa na hayo.

Itanibidi kuacha amana ninapochukua gari langu?

Ndio. Wakati wa kuchukua gari, mhudumu wa kaunta atakuhitaji uwache amana pengine gari lako litaharibika au kuibiwa wakati wa ukodeshaji wako. Kiasi hicho cha amana kitazuiliwa kwenye / kuondolewa kutoka kwenye kadi ya malipo ya dereva mkuu na kushikiliwa kwa kile kipindi cha huo ukodeshaji.

Mradi unarejesha gari likiwa halijaharibika mwishoni mwa ukodeshaji, pesa hizo zitafunguliwa / kurudishwa ndani ya siku saba za kikazi.

Ikiwa kadi ya malipo ya dereva wako mkuu haina pesa za mjazo za kutosha kuweka amana, huenda usiruhusiwe kuchukua gari – au mhudumu wa kaunta huenda akasisitiza ununue usimamiaji wa ziada kutoka kwao.

Hili ni jambo linalotendwa kimsingi na makampuni yote ya ukodeshaji magari.

Ni usimamiaji mgani wa ziada ninaoweza kununua kutoka kwa mhudumu kwenye kaunta?

Makampuni mbali mbali ya ukodeshaji gari huenda yakauza aina mbali mbali za usimamiaji, lakini ule unaofanyika sanasana ni Ondoleo Kuu la Gharama ya Uharibifu kwa Mgongano (SCDW). Kulingana na kampuni, sheria ya SCDW yaweza:

 • Kusimamia sehemu za gari ambazo hazijasimamiwa na sheria ya usimamiaji wa kawaida wa hilo kampuni Ondoleo Kuu la Gharama ya Uharibifu kwa Mgongano (madirisha na magurudumu, kwa mfano)
 • Hupunguza yale ya ziada – na kupunguza kiasi cha juu zaidi ambacho inakubidi ulipe ikiwa uliharibu kitu ambacho kimesimamiwa na bima ya gari
 • Weka vya ziada kwa sifuri, ili isikubidi kuwacha amana wakati wa kuchukua gari – au kulipa chochote kwa ajili ya uharibifu wa kitu ambacho kimesimamiwa na bima ya gari.