Skip navigation links
rentalcars
 Akaunti yangu
Funga
Je, umesahau rejeleo lako la uhifadhi?

Ingiza anwani yako ya barua pepe na tutakutumia nambari yako ya rejeleo kwa anwani hii.

Barua pepe imetumwa.

Umetumiwa rejeleo lako la uhifadhi kwa barua pepe.

Nambari ya rejeleo haikupatikana

Hatujaweza kupata uhifadhi wa sasa kwa kutumia anwani hii ya barua pepe. Tafadhali Wasiliana Nasi kwa kutumia kiungo hiki

Ingiza tena anwani ya barua pepe.

Karibu kwa Rentalcars.com

Utajihisi vyema zaidi – gurumisha injini na msisimko wako umeanza…

Katika Rentalcars.com chote tufanyacho ni kukupa uhuru wa kugundua mengi. Tutaondoa vizuizi vyote ili kukupa gari linalofaa la kukodesha, na kukuletea ujuzi wa mtiririko, usio na bughudha kuanzia mwanzoni hadi mwisho. Hapa unaweza kugundua mengi zaidi kuhusu jinsi tunavyofanya kazi.

Mambo tunayoshughulika nayo

Tungependa kufanya ukodeshaji wa gari kuwa rahisi na wa kibinafsi kana kwamba unaendesha gari lako mwenyewe.

Ukodeshaji gari unaokupa uhuru, na tutakusaidia kupata gari lifaalo kwa bei nafuu zaidi. Lakini kuna mengi zaidi kutuhusu kando na hayo. Tuko hapa ili kufanya ukodeshaji gari kuwa bila bughudha.

Twajua kwamba ubora wa huduma unayopokea ni muhimu sana

Kwa hivyo tunatumia maoni halisi na halali ya wateja, na ujuzi wetu wenyewe ili kukuelekeza kwenye chaguo bora zaidi.

Tunafanya kazi na makampuni ya ukodeshaji magari kote ulimwenguni

Kuanzia kwa majina ya kinyumbani hadi makampuni madogo ya kinyumbani – ili kukuletea magari , chaguo na dili zitakazofanya safari yako kuwa ya kipekee.

Na tutakuwa nawe katika kila hatua

Timu yetu kwa wateja itakusaidia katika safari yako, kokote na wakati wowote unaohitaji usaidizi.

Jinsi tunavyofanya kazi

Kuhakikisha unapata ujuzi mpya kila mara unapokodesha gari hutapatia furaha.

Sisi ni mawakala, kwa hivyo tunaandaa ule ukodeshaji gari kwa niaba yako. Tunatumia uweza wetu mkuu wa ununuzi ili kukuletea dili nzuri zaidi. Lakini sisi ni zaidi ya tovuti ya kulinganisha bei, kwa sababu tutakuwa nawe katika kila hatua.

 • Durusu Durusu tovuti yetu au app kwa lile gari unalotaka

 • Linganisha Tunakuonyesha dili na maoni unayohitaji ili kukusaidia kuchagua

 • Tuma maombi Chagua gari unalotaka, ongezea chochote cha ziada unachotaka – kama vile Bima Kamili (usimamiaji wetu wa ziada) au kiti cha gari – na utume maombi

 • Uko sawa sasa Tutathibitisha utumaji maombi wako kwa lile kampuni la ukodeshaji gari ulilochagua, na kukuthibitishia wewe

 • Chukua gari lako Chukua vocha (kwenye karatasi au kwenye app yako), kadi yako ya kulipia deni, leseni ya uendeshaji gari na pasipoti ili kuchukua gari lako

 • Kuwa na safari ya kupendeza Endesha gari na uanze kugundua mengi…

 • Furahia usaidizi wetu Tuko hapa masaa 24/7 ili kukusaidia – kabla, wakati na baada ya safari yako

Mbona ututumie sisi

Kwa maneno mengine, kwa sababu tunakuletea thamani kubwa zaidi na amani ya mawazo katika safari yako ya ukodeshaji gari.

Tunatumia ujuzi wetu wote – na ujuzi wa mamilioni ya wateja –ili kukuletea gari unalohitaji na ubora wa huduma unayohitaji. Daima kwa bei bora zaidi. Lakini usiitikie neno letu tu. Jiangalilie vile watu halisi wanafikiria kuhusu Rentalcars.com.

Trustpilot

Tulikadiria 8.1 kati ya 10 kwenye Trustpilot kulingana na ukaguzi 64,810.

World Travel Awards 2016

Tovuti Bora Zaidi Ya Uingereza Ya Ukodeshaji Gari

Travolution Awards 2015

App Ya Kampuni Inayoongoza Duniani Ya Ukodeshaji Gari

Sisi ni kina nani

Waanzilishi wetu walikuwa na wazo la kutaka kuboresha ukodeshaji gari. Na tumenawiri kwa sababu wateja wetu hupenda jinsi tunavyofanya kazi.

Tulianza mwaka wa 2004 kwenye TravelJigsaw. Miaka mine baadaye, tulikuwa tukipata maombi 1000 kwa siku. Mnamo 2010, tulijiunga na Priceline Group na tukabadilisha jina likawa Rentalcars.com.

Leo hii tunapata maombi milioni 8.5 kwa mwaka (na yanazidi kuongezeka) katika maeneo 53,000 katika nchi 163.

Ukuaji wetu wa kustaajabisha unategemea timu yetu ya watu wazuri. Sisi ni washirika 1200 kutoka nchi 70 na makao yetu yako Manchester, Uingereza.

Tunajivunia kuwa sehemu ya familia inayoongoza mtandaoni kwa bidhaa za usafiri ulimwenguni:

 • Booking.com
 • Priceline
 • Kayak
 • Agoda.com
 • Rentalcars.com
 • OpenTable